Monday, April 17, 2017

SOMO LA 001: MAANA YA VIONGOZI MAKINI(ALPHA NETWORKERS):

Habari yako Rafiki?
Karibu Sana kwenye kipindi hiki cha Leo. Hongera pia kwa kuchukua Maamuzi ya Kuongeza Maarifa Yako. Tumejaliwa Leo ili Tuboreshe Maisha yetu kwa kuwa Na bidii.

Ndio Networker ni Mtu anawaelewa watu, anawaeleza na kuwaelimisha Watu kuhusu bidhaa na mfumo wa kampuni Fulani la Biashara Ya Mtandao (Network Marketing Companies).

Pia Ni Mnunuzi wa jumla wa bidhaa Katika kampuni husika. Huuza kwa rejareja bidhaa Hizo.

AINA ZA NETWORKER( BALOZI WA KAMPUNI)

(a) Wafuasi (Beta Networkers)

(b) Viongozi Watarajiwa(Pre-alpha Networkers)

(c) Viongozi Makini (Alpha Networkers)


TABIA ZA WAFUASI (BETA NETWORKERS)

Kwanza wana ujasiri kidogo Sana au hawana kabisa hata kama Hamna anaewatazama kwa muda huo.

Mara nyingi ni bendera fuata Upepo hata kama hana sababu ya Kufanya huyu hufanya ili kuepuka kuwa tofauti na wengine.

Hawana uhakika na kila wanalolifanya hata kama yupo sahihi. Kila linalotokea katika Maisha yake humpelekea Lawama mtu Fulani.

TOFAUTI kubwa Kati ya Wafuasi na viongozi Watarajiwa ni Kuwa Viongozi Watarajiwa wana Maono, Wanajipa Moyo na kuhitaji Kufanya vitu muhimu kuhusu Maisha yao.


TOFAUTI KATI YA VIONGOZI WATARAJIWA NA VIONGOZI MAKINI.

Viongozi Makini(alphas) wana mvuto kwa wengine bila kujali kupingwa kwao Lakini Pre-alphas Hawana Mvuto kwa wengine.

Alphas Wanajua kabisa nini wanahitaji kwenye Maisha yao kama ni udaktari,  ualimu, na uanajeshi, huyu alphas ataimba hiyo Kazi yake mpaka anakufa. Lakini Pre-alphas (Viongozi Watarajiwa)  wana Maono aynayoyumba anaweza kukuambia Leo Ualimu kesho, Udaktari.

Alphas (Viongozi makini) hufauta Sana sheria katika Maisha yao, asipofanya hiyvo huona ametenda kosa kubwa sana. Lakini Pre-alphas sio lazima wafuate sheria ili kuendesha Mambo ya

Alphas wananguvu ya kufuatilia ndoto zao kila kunapokucha. Lakini Pre-alphas Hana Habari yoyote juu ya ndoto zake yeye hujifariji tu kuwa Ipo Siku atapata hata kama hafanyi lolote juu ya Ndoto zake.


Mimi na Wewe Tunahitaji Tuwe Alphas(Viongozi makini). Haijalishi wewe ni mfanyabiashara, mwanasiasa, kiongozi wa Dini,  Mwalimu, Daktari na hata mfagia takataka barabarani.

Sisi Sote tunahitaji kuwa Viongozi makini (Alphas),  hii itakusaidia Sana kujenga Maisha yetu kwa Ujumla. Huwezi Unafanikiwa kwa Njia halali kama wewe ni Betas au Pre-alphas.

Ndio Sababu nikaandika Sisi tutaitwa Alphas Kwa Sababu tutajifunza Hatimaye kuwa sehemu ya mafanikio.

Hongera Sana kwa makala  ya  Leo ninaamini Umejinza kitu. KUMBUKA Tunaongelea Biashara Ya Mtandao (Network Marketing businesses)

Karibu tena katika kipindi kijacho,


Ni Mimi Rafiki yako,

ALIKO MUSA.


Barua Pepe : alikomusa255@gmail.com

BLOG : www.ardhinamajengo.blogspot.com

              www.alikorealestate.blogspot.com

No comments:

Post a Comment